Social Icons

Pages

Suzane

Suzane

Featured Posts

Wednesday, 17 June 2015

PATA KUJUA DESIGN MPYA ZA MAGAUNI YA HARUSI MWAKA 2015

 Hizi Ndio Design Mpya na Hazina Maurembo sanaaa kwa Wale Wanaopenda Simple na Unique
 Hapo Akionesha Nakshi ya Gauni Lake Kwa Nyuma. 
 Gauni Hili Sehemu kubwa ni Lace na  inakukaa sawa na mwili wako .......Hatariiiiiii
Hii pia ni Design Mpya ni Nzuriiiiiiiiiiii
 Amenogaaa mnoooo unakosaje Kujua Gauni gani  utavaa na madesigner wanatutolea vitu vizuri Hivi
 Yaani LACE ndio Habari ya mjini

 Amazing..........

 More Design tushindwe vip kunoga kwenye Harusi zetu Wapendwa
 LACE Bado inakimbiza  dada amependeza mnoooooo
 Ni zaidi ya WOOTE Daaah  Haya Magauni ni Mazuri sana
MPENDWA usiache Kupendeza siku ya Harusi yako Maana Haitojirudia Kamwe.                              Karibu Uone na UJIFUNZE Kila Kinachohusiana na Harusi Hapa Kwetu  .

RANGI ZA HARUSI KWA MWAKA 2015

Hizi ndizo Rangi Ambazo Zimependwa na Kutumiwa Sana Kwenye Maharusi Tangu tuuanze Mwaka HUU 2015

Kama Zionekanavyo ni Rangi Nzuri na zimepoa huvutia Sanaaa Zipambwapo

Mchanganyiko huu wa Rangi umependezesha kila kitu....... Mandhari tulivu yaani Simply Beautiful

Thursday, 9 October 2014

UBUNIFU KATIKA HARUSI..!! WAMAREKANI WAFUNGA NDOA JUU YA MLIMA KILIMANJARO.

Kara Lee akimvisha pete mumewe Richard Miller.
Wanandoa hao waliwasili nchini wiki iliyopita na kuanza safari yao ya siku saba kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Machame Septemba 20, 2014 na kutumia usiku huo katika banda la Machame.
Kara Lee anasimulia hivi: “Katika Sikukuu ya Krismas huko Minnesota nchini Marekani tulivishana pete mimi na mchumba wangu Richard Miller na kuwekeana ahadi kuwa ndoa yetu lazima ifungwe juu ya paa
la Afrika na hiyo sehemu si nyingine zaidi ya Mlima Kilimanjaro”.
Wanandoa hao wakisaini kitabu cha maharusi.
Baada ya hapo, wawili hao walianza mipango ya kutimiza ndoto yao hiyo ya pekee na ya kihistoria kwa kukusanya fedha kwa ajili ya safari yao kuja Tanzania. Wapenzi hao waliwajulisha ndugu na jamaa juu ya uamuzi wao huo ambapo walipata baraka zote za kutimiza ahadi hiyo.
Safari yao ya kupanda mlima huo ilikuwa ikiongozwa na Kampuni ya Utalii ya Zara iliyopo mjini Moshi, Kilimanjaro ambapo Septemba 21 mwaka huu majira ya saa 6 mchana wawili hao waliwasili katika pango
la Shira wakitokea banda la Machame wakiwa pamoja na wenyeji wao tayari kwa ndoa yao hiyo iliyokuwa gumzo kwa watu waliohudhuria.
Mchungaji Aloyce Mbugi kutoka Kanisa la TAG la Victory Christian Centre lenye makazi yake jijini Arusha akiwafungisha ndoa Kara na Richard.
Siku hiyo ya Jumapili, Septemba 21, 2014 Mchungaji Aloyce Mbugi kutoka Kanisa la TAG la Victory Christian Centre lenye makazi yake jijini Arusha alianza ibada ya kuwafanya kitu kimoja Richard Miller na Kara Lee kama mume na mke.
Maharusi hao wakisimamiwa na Ansigar Mtandika na Neema Njau, walianza kula viapo vya ndoa pamoja na kuvishana pete mbele ya mchungaji huyo huku wakiahidi kuwa pamoja katika shida na raha mpaka
Mwenyezi Mungu atakapowachukua.
Wanandoa hao katika pozi baada ya kufunga ndoa.
Baada ya zoezi hilo, wanandoa hao walikunywa shampeni pamoja na waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria na kuhitimisha ndoa hiyo iliyofungwa kwa saa tatu.
Richard na Kara walianza maisha ya mke na mume katika hema na leo wameendelea na safari yao ya kuupanda mpaka kileleni Mlima Kilimanjaro ambapo wamefika kituo cha Baranco. Wanandoa hao
wanataraji kufika kilele cha mlima huo kesho Jumatano na wataanza kushuka kuelekea geti la Mweka Keshokutwa Alhamisi ya Septemba 25, 2014.

“Wana nguvu na wamepania kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro na naamini watatimiza ndoto yao nyingine hiyo," alisema Teophil Karia, mwongoza wageni kutoka Zara Tours.

YAJUE MATUKIO MUHIMU KATIKA HARUSI..!!!

NDOA
UKUMBI, ni Vyema ukapambwa kwa rangi zinazofanana na RANGI YA HARUSI..!!


KUMBUKUMBU, Kumbuka kuwapa kazi hii muhimu watu makini sana kwani Tukio hili halitajirudia kamwe..!!

USAFIRI, Hakikisha swala la usafiri limekaa sawa, Msafara wa Maharusi ni vyema ukaongozana na wapambe

CHAKULA, Shirikisha wapishi wanaofanya kazi hiyo kwa umakini

FUNGATE, Ni muhimu kupata mapumziko  baada ya shughuri




UBUNIFU, HARUSI AINA YAKE YAFUNGWA NDANI YA MAJI, ZIMETUMIKA MAKE-UP ZISIZOHARIBIWA NA MAJI

Katika mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.

Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii.Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.

Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.

Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.

'Mtindo tofauti wa picha'
''Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.
"maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ''

Tina Liu mmiliki wa duka la Mr Wedding
Hawa ni wateja wake, Lin Enxiao na He Huan.
Ndoa yao haijawa tayari kwani wataoana mwaka ujao, lakini wapenzi wengi wachina wanasema wameamua kujipiga picha zao za harusi mapema ili wasipate tatizo lolote.
''Marafiki wetu wengi walijipiga picha katika eneo kavu,'' asema YY. "sisi tulitaka kitu tofauti. ''
Watu wanapofikiria kuhusu picha za harusi, wao hutaka kujipiga sehemu kavu kuliko kuta nyeupe au nyasi, '' asema Lamea.
"sisi tunahisi vyema kubadili mtindo huo.''
Kisha maharusi hawa wanatembezwa na kuingizwa ndani ya tenki ya maji ambako wanapigiwa picha.
Tenki hiyo huwa na maji ya vuguvugu na mtu wa kuwasidia maharusi pia huwa ndani ya tenki hiyo ambamo wanapigiwa picha.
Tina alianza kazi hii mwaka 2003 wakati huo akipiga picha tu za kawaida za harusi kabla ya kuanza kuwapiga picha watu wakiwa ndani ya maji.

Kila biashara zina changamoto zake. Kwa Tina lazima awe na maarifa ya utenda kazi ili kazi yake iweze kunawiri.

MAVAZI NA MITINDO YA KIAFRIKA KATIKA HURUSI..!!

Anameeeremeeetaaaaaa..anameremeeeeeta Bibi Harusi ana Meremeeeta anaaaa....!!!

Niceeeeeeee...Ubunifu katika Harusi..Kiafrica zaidi hata viatu havihusiki..

Bwana na Bibi Harusi wakipata picha ya kumbukumbu

Mitindo na Mapooouuuzzzzz..!!

Bwana na Bibi harusi ndani ya African Print sooooo....Mwaaahhh!!

African House Cake

HONGERA MISSIE POPULAR - MARIAM MARION NDABA SEND OFF PARTY

Missie popular night,last night. gauni kutoka kwa Eve Collection..makeup by Glambox... ama kwa hakika AMETOKLEEZEAAAAA...!! Picha za Tukio zima zitafuata hivi punde..