Katika
mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa
kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika
eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu
kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza
kufanyika hapa.
Duka
lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo
inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko
nyinginezo katika historia ya nchi hii.Biashara hii ni moja ya biashara
ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Kulingana
na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa
zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na
thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.
Duka
hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha
mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba
maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
'Mtindo tofauti wa picha'
''Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.
"maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ''
|
No comments:
Post a Comment