Wanandoa hao katika pozi baada ya kufunga ndoa.
Baada ya zoezi hilo, wanandoa hao walikunywa shampeni pamoja na
waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria na kuhitimisha ndoa hiyo
iliyofungwa kwa saa tatu.
Richard na Kara walianza maisha ya mke na mume katika hema na leo
wameendelea na safari yao ya kuupanda mpaka kileleni Mlima Kilimanjaro
ambapo wamefika kituo cha Baranco. Wanandoa hao wanataraji kufika
kilele cha mlima huo kesho Jumatano na wataanza kushuka kuelekea geti la
Mweka Keshokutwa Alhamisi ya Septemba 25, 2014.
“Wana nguvu na wamepania kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro na
naamini watatimiza ndoto yao nyingine hiyo," alisema Teophil Karia,
mwongoza wageni kutoka Zara Tours. |
No comments:
Post a Comment